Jerry J Mbwille
July 20, 1979 - February 17, 2022
Kuzaliwa: Jerry alikuwa ni mtoto wa 3 kati ya watoto 4 wa marehemu Judith Mbwille na Kanali Jackson Mbwille (mstaafu). Jerry alizaliwa Julai 20, 1979 huko Bugando Mkoani Mwanza, Tanzania. Elimu Na Kazi Jerry alisoma shule ya Msingi Mbuyuni na Forodhani Dar-es-Salaam na akaenda Jitegemee Secondary School, na St. Mary’s High School. Baada ya kumaliza shule, Jerry alikwenda Marekani kuhitimu elimu yake ya juu. Jerry alisoma international business administration katika vyuo vya Strayer University, huko Washington DC na St. Cloud State University Minnesota. Jerry alifanya kazi Curries huko Mason City, Iowa na pia alikuwa mjasiriamali huko Tanzania mpaka mwisho wa maisha yake. Katika maisha yake, Jerry alikuwa ni kijana mwelevu sana na mwenye hekima,upendo kwa ndugu, jamaa na marafiki. Kwa lugha ya kinyumbani, tunasema Jerry alikuwa mtu wa watu. Jerry alikuwa ana mpango wa kurudi nyumbani Tanzania ili kufungua ukurasa mwingine wa maisha yake. Mpango mkubwa ni kuendeleza biashara ya Nguruwe mama yetu aliouacha, hii ni kwa sababu yeye ni mtawala (Administrator katika Familia) Jerry hakuwa na watoto au mke, ila watoto wa ndugu zake alikuwa anawadekeza na kuwapenda sana kama watoto wake mwenyewe. Maradhi: Jerry hakuwa na matatizo ya kiafya, wiki moja kabla ya mauti alisema ana mauvi ya misuli ya miguu , na yalipita ,na kuendelea na shughuli zake. Siku ya Alhamisi asubuhil alisema tumbo linauma anasikia kutapika lakini anashindwa na anaishiwa pumzi ndiyo walipoita Ambulance na kumpeleka Hospitali ndiyo umauti ulimkuta. Shukrani: Familia ya Kanali Mstaafu Jackson Mbwille wanatoa shukrani za dhati kwa jumuiya ya Tanzania, Iowa, Minnesota, Hogan Bremer Moore Colonial Chapels, kwa maombi yao na maandalizi ya kumpeleka Jerry katika makao yake. Wanafamilia wanatoa shukrani zao za dhati kwa jopo la madaktari wa hospitali ya Mercy, Mason City, Iowa ambao walimhudumia Jerry katika jitihada za kuokoa maisha yake mpaka umauti ulipomfika Pia wanafimilia wanatoa shukrani za dhati kwa ndugu jamaa marafiki na majirani na wale, wote walitoa misaada ya hali na mali katika jitihada za kufanikisha shughuli nzima ya mazishi ya ndugu yetu mpendwa Jerry Mbwille, Mungu awabariki.
Kuzaliwa: Jerry alikuwa ni mtoto wa 3 kati ya watoto 4 wa marehemu Judith Mbwille na Kanali Jackson Mbwille (mstaafu). Jerry alizaliwa Julai 20, 1979 huko Bugando Mkoani Mwanza, Tanzania. Elimu Na Kazi Jerry alisoma shule ya Msingi Mbuyuni... View Obituary & Service Information